Qatar inatumai viongozi wanaoshiriki mkutano huo wa dharura watakuja na mbinu ya kuizuwia Israel wakati ikiendeleza vita vyake dhidi ya Hamas katika Ukanda wa Gaza. 

Shambulizi hilo limekuja wakati Qatar ikiwa ni mpatanishi muhimu katika juhudi za usitishwaji vita, jambo ambalo Doha imesema itaendelea kulifanya hata baada ya shambulizi hilo.

Waziri Mkuu wa Qatar, Sheikh Mohammed bin Abdulrahman Al Thani ambaye pia ni waziri wa mambo ya nchi za nje wa taifa hilo, ameitolea wito dunia kuachana na kile alichosema ni “undumilakuwili” na kuiadhibu Israel.

“Tunashukuru kwa hatua ya kuilaani Israel na kuonyesha mshikamano na Qatar, kwa kuunga mkono uhuru wetu, mamlaka yetu, na kuunga mkono jukumu letu la kuwa mpatanishi. Leo, lazima tuchukue hatua madhubuti kukomesha kiburi cha Israeli na kuendelea kwake kufanya uhalifu dhidi ya binaadamu chini ya hatua ya undumilakuwili  kutoka kwa Jumuiya ya kimataifa. Amani iwe juu yenu na rehema za Mwenyezi Mungu na baraka zake.”

Tangu Hamas ianzieshe mashambulizi ya Oktoba 7 mwaka 2023 nchini Israel, yaliyochochea mgogoro ulioko sasa Mashariki ya Kati, Israel tayari imezishambulia Iran, Lebanon, Syria, Qatar na Yemen.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *