
Ushindi huo unatokea wakati chama kinachofuata siasa kali za mrengo wa kulia, AfD, kikiongeza umaarufu wake kwa asilimia 5 ikilinganishwa na uchaguzi uliopita wa mwaka 2020.
Merz aliyeigia madarakani mwezi Mei na ambaye chama chake kimetabiriwa kuongoza kwa asilimia 33.3 amesema chama chake kimeibuka kuwa imara kwa kutatua matatizo ya wajerumani hasa katika uchumi, uhamiaji, na usalama.
Uchaguzi huyo ni kipimo cha kwanza debeni kwa serikali ya muungano ya Kansela Merz inaojumuisha muungano wa kihafidhina wa vyama vya Christian Democratic Union, CDU, na Christian Social Union, CSU, na Chama cha siasa za wastani zinazoegemea mrengo wa kushoto cha SPD.