Charles Mwesigwa - anayejulikana kwa jina la Abbey - anasema wanawake wanaomfanyia kazi ni machachari sana

    • Author, Runako Celina
    • Nafasi, BBC Eye Investigations

Tahadhari: Ina maudhui na maelezo ya matukio ya ngono

Uchunguzi wa BBC umefichua mwanamume anayeendesha mtandao wa biashara ya ngono kutoka kwenye maeneo ya kifahari ya Dubai, akiwanyanyasa wanawake walio katika mazingira magumu.

Mwanamume huyo, anayeitwa Charles Mwesigwa, ambaye anadai kuwa alikuwa dereva wa basi jijini London, aliiambia mwandishi wa BBC aliyekuwa akifanya upelelezi kwa siri kuwa anaweza kupanga wanawake kwa ajili ya sherehe za ngono, kuanzia bei ya dola 1,000 kwa kila mwanamke.

Aliongeza kuwa wanawake hao wanaweza kufanya karibu kila kitu mteja anachotaka.

Kwa miaka mingi, kumekuwepo na tetesi kuhusu sherehe chafu za ngono huko Dubai.

Hashtag maarufu #DubaiPortaPotty ambayo imeangaliwa mara milioni 450 imeenea kwenye mitandao ya kijamii, hasa TikTok, ikihusishwa na wanawake wanaodaiwa kukubali kufanyiwa matendo ya udhalilishaji wa kingono kwa malipo makubwa.

Lakini uchunguzi wetu wa BBC umebaini hali ya kusikitisha zaidi ya ile inayosikika mitandaoni.

Wanawake wachanga kutoka Uganda waliambia BBC kuwa walihadaiwa na hawakutarajia kufanya kazi ya ngono inayosimamiwa na Mwesigwa.

Kwa baadhi waliamini wanasafiri kwenda kufanya kazi katika maduka au hoteli huko uarabuni, lakini walipoingia Dubai, waliishia katika biashara ya ngono inayoendeshwa na Mwesigwa.

Mmoja wao, tunamwita Mia (si jina lake halisi), anasema alilazimishwa kufanya kazi hiyo na aliambiwa kuwa ana deni la zaidi ya paundi 2,000, ambalo lilikua hadi mara mbili ndani ya wiki mbili tu. Alieleza kuwa wateja wengi walikuwa raia wa Ulaya wenye matamanio ya kingono yaliyopitiliza.

Angalau mmoja wa wateja wa Bw Mwesigwa huomba kuwapaka kinyesi wanawake hao, kulingana na “Mia”, ambaye jina lake tumelibadilisha ili kulinda utambulisho wake, na ambaye anasema alinaswa katika himaya ya Bw Mwesigwa.

Hata hivyo Mwesigwa anakanusha madai hayo.

Anasema anawasaidia wanawake kupata makazi kwa njia ya wamiliki wa nyumba, na kwamba wanawake wanamfuata katika sherehe za kifuska kutokana na uhusiano wake na mabwenyenye wa Dubai.

Tumegundua kwamba wanawake wawili wanaohusishwa na Mwesigwa wamefariki dunia, waliporuka kutoka majengo ya juu.

Ingawa vifo vyao vilihukumiwa kuwa mauaji ya kujitia kitanzi, marafiki na familia yao wanaona kwamba polisi wangepaswa kuchunguza kwa kina zaidi.

Bw Mwesigwa alisema matukio hayo yalichunguzwa na polisi wa Dubai na kutuomba tuwasiliane nao kwa taarifa zaidi kilichojiri.

Walakini hawakujibu ombi letu.

Pia unaweza kusoma:

Mmoja wa wanawake waliopoteza maisha, Monic Karungi, alifika Dubai kutoka magharibi mwa Uganda.

Alijikuta akiishi katika nyumba ya pamoja na wanawake wengine wengi wanaofanya kazi kwa Mwesigwa, kulingana na mwanamke mmoja tunayeita Keira, ambaye anasema aliishi na Monic katika nyumba hiyo mwaka 2022.

“Makaazi yake ilikuwa kama soko… Kulikuwa na wasichana kama 50. Alikuwa hana furaha kwa sababu kile alichotegemea si kile alichopata,” Keira alituambia.

Monic alifikiri kazi Dubai ingekuwa yoyote ya duka la jumla, kulingana na dada yake Rita.

“Mwesigwa alikuwa mkali nilipomwambia nataka kurudi nyumbani,” anasema Mia, ambaye pia alimfahamu Monic wakiwa Dubai. Anasema alipofika tu mara ya kwanza, Mwesigwa alimwambia alikuwa anamdai tayari paundi 2,000 ($2,711), na ndani ya wiki mbili deni hilo liliongezeka mara dufu.

“Pesa za tiketi ya ndege, visa yako, malazi yako, chakula,” Mia anasema.

“Yaani lazima ufanye kazi ngumu, kama kubembeleza mwanamume aje mfanye ngono zembe.”

Monic alidai Mwesigwa zaidi ya $27,000 (paundi 19,918) baada ya wiki kadhaa, kulingana na taarifa ya ndugu yake anayefahamika kwa jina Michael. Anasema alipokea sauti zenye kulia kutoka kwake.


Monic anatabasamu kwenye kamera - amevaa blauzi ya rangi ya manjano na nyeupe

Chanzo cha picha, Family handout

Mia alituambia kwamba wateja mara nyingi ni wazungu wa Ulaya, na baadhi wao wana tabia za ngono ambazo watu wengi wanaona kuwa zisizo za kawaida.

“Kuna mteja mmoja, anaenda haja kubwa juu ya wasichana. Akimaliza shughuli anawaambia wale kinyesi chake,” alieleza kwa sauti ya chini.

Mwanamke mwingine, tunayempa jina Lexi ambalo si lake halisi, anasema alihadaiwa na kampuni tofauti, alithibitisha simulizi ya Mia, akisema miamala ya “porta potty” ilikuwa ya kawaida.

“Kulikuwa na mteja alisema: ‘Tunakulipa Dirham 15,000 za Falme (takriban $4,084, paundi 3,013) kukubaka kama kundi, tupate haja kubwa juu yako, tukupige na tukuongeze Dirham 5,000 ($1,361, paundi 1,004)” kwa kurekodiwa ukikula kinyesi.

Uzoefu wake umemfanya aamini kuna sehemu ya ubaguzi wa rangi katika tabia hizi za ngono zisizo za kawaida.

“Kila nilipo sema siwezi kufanya hivyo, inaonekana wao wanafurahia zaidi. Wanataka mtu atakayelia, apige mayowe na pia ajaribu kukimbia. Na mtu huyo [kwa macho yao] aonekane ni asili ya Kiafrika.”

Lexi anasema alijaribu kutafuta msaada kutoka kwa watu ambao alihisi wangemsaidia- polisi.

Lakini polisi walisema: “Nyinyi Waafrika mnapenda kubandikizana matatizo Hatutaki kujihusisha.” Wakakata simu yao.

Tulimweleza polisi wa Dubai mashtaka haya, lakini hawakujibu.

Lexi hatimaye alitoroka kurudi Uganda na sasa husaidia kuokoa na kusaidia wanawake katika hali kama hiyo.

Warsan Tower, mnara mrefu sana wa rangi ya fedha huko Dubai

Kumpata Charles Mwesigwa haikuwa rahisi.

Tuliweza kupata picha moja tu mtandaoni na ilikuwa imechukuliwa kutoka mgongo. Pia anatumia majina tofauti kwenye mitandao ya kijamii.

Lakini kwa kutumia taarifa za wazi, upelelezi wa siri, na taarifa kutoka kwa mtu aliyekuwa sehemu ya mtandao wake, tumemfikia katika eneo la tabaka la kati la Dubai – Jumeirah Village Circle.

Ili kuthibitisha yale tuliyoyaambiwa kuhusu biashara yake – ya kuwauzia wateja wake wanawake kwa matendo ya ngono ya unyanyasaji – tumemtumia mwandishi wetu kama mratibu wa hafla akijifanya anatafuta wanawake kwa sherehe ya kifahari.

Mwesigwa alionekana mtulivu na kujiamini alipokuwa akizungumza kuhusu biashara yake.

Picha iliyonaswa na kamera ya siri ya Charles Mwesigwa. Anatazama chini na amevaa juu nyeusi na nyeupe yenye mistari wima. Chini ya sura ni sehemu ya kile kinachoonekana kuwa leseni yake ya kuendesha gari ya Uingereza.

“Tuna wasichana kama 25,” alisema. “Wengi ni wajanja… wanaweza kufanya karibu kila kitu.”

Alielezea gharama – kuanzia $1,000 (paundi 738) kwa kila msichana kwa usiku mmoja, lakini zaidi kwa “mambo yasio ya kawaida ya kichachari”. Alimwalika mwandishi wetu kwa “usiku wa majaribio.”

Alipoulizwa kuhusu “Dubai porta potty” alijibu: “Nimesema tayari, ni wajanja. Ninaposema ni machachari… nitakutumia walio na machachari zaidi.”

Katika mazungumzo, Mwesigwa alisema alikuwa dereva wa basi London.

Tumeona ushahidi kwamba alizitaja kazi hiyo katika hati rasmi huko London Mashariki mwaka 2006.

Aliongeza kuwa anapenda biashara hii.

“Ningeshinda bahati nasibu, paundi milioni moja, lakini ningekuwa nikiendelea kufanya hivi… imekuwa sehemu yangu.”

Troy, mtu anayesema alikuwa meneja wa shughuli kwa kazi ya Mwesigwa, alitupa taarifa zaidi kuhusu jinsi anavyosema inavyoendeshwa.

Troy is wearing a black bobble hat, cream collared-top, has a beard and an earring and a distinctive anchor tattoo on his forehead

Anasema Mwesigwa hulipa walinzi katika vilabu mbalimbali usiku ili wanawake wake waingie na waweze kutafuta wateja.

“Nimesikia kuhusu aina ya ngono ambayo sijawahi kuona katika maisha yangu. Haijalishi unatendewa nini mradi wanaume wake matajiri wafurahie… [wanawake] hawana njia ya kutoroka… Hukutana na wanamuziki, wachezaji wa soka, na hata marais.”

Mwesigwa ameweza kuendesha shughuli hii, Troy anadai, kwa sababu Troy na wengine hawatumiki tu kama madereva. Anasema majina yao hutumiwa pia na Mwesigwa kukodisha magari na makazi, ili jina lake halijitokezi kwenye hati.

Mnamo 27 Aprili 2022, Monic alipakia picha yake mwenyewe kutoka Al Barsha – eneo la makazi lenye watu wengi kutoka nje huko Dubai.

Siku nne baadaye, alipoteza maisha. Alikuwa amekaa Emirate kwa miezi minne tu.

Kulingana na Mia, Monic na Mwesigwa walikuwa wakipigana mara kwa mara kabla ya kufariki.

Mia anasema Monic alikuwa amekataa kutekeleza matakwa ya Mwesigwa na alikuwa ameanzisha njia ya kutoka kwenye biashara hiyo.

“Alikuwa ameajiriwa kazi fulani. Alifurahi sana. Alifikiri angepata uhuru, angepata maisha yake tena kwa sababu hiyo ilikuwa kazi halisi sasa, hakuna kulala na watu wa jinsia ya kiume,” Mia anasema.

Monic alihamia kwa nyumba nyingine umbali wa takribani dakika 10 kwa miguu. Kutoka roshani ya nyumba hiyo inadaiwa aliruka tarehe 1 Mei 2022.

Video ya mtandao wa kijamii ya Monic ikimuonyesha mwanamke kijana akitazama kamera na nywele nyeusi zilizokatwa moja kwa moja hadi mabegani mwake na kwa pindo.

Chanzo cha picha, Instagram

Ndugu wa Monic, Michael, ambaye alikuwa Dubai wakati akifariki, anasema alijaribu kupata majibu ya kilichotokea.

Polisi walisema walimaliza uchunguzi baada ya kugundua dawa za kulevya na pombe katika chumba cha nyumba ambayo Monic alikuwa ameruka, na alama za vidole za Monic pekee kwenye balcony, anasema.

Alipata cheti cha kifo kutoka hospitali kwa Monic, lakini haikutaja ni jinsi gani alikufa. Familia yake haikuweza kupata ripoti ya kiwango cha kusumisha kwake.

Lakini mwanaume kutoka Ghana aliyeishi katika jengo la nyumba alisaidia zaidi, alimpeleka kwa jengo lingine kukutana na mtu anayesema ndiye bosi wa Monic.

Michael anaelezea alichokiona alipofika na kuona wapi wanawake waliishi.

Anasema kupitia moshi wa shisha katika sebuleni, aliona kile kilichoonekana kuwa kokeini juu ya meza na wanawake wakifanya ngono kwa viti na wateja.

Anadai alimkuta mtu tuliyemtambua awali kama Charles Mwesigwa kitandani na wanawake wawili, na alipomjaribu kumpeleka polisi Mwesigwa alijibu: “Nimekuwa Dubai kwa miaka 25. Dubai ni yangu… Huwezi kuniripoti… Ubalozi ni mimi, mimi ni ubalozi.”

“[Monic] si wa kwanza kufa. Na hatakuwa wa mwisho,” aliongeza, kulingana na Michael.

Mia na Keira wanathibitisha kwa njia tofauti walisikiliza mazungumzo haya na wote wanakubaliana na maneno yaliyotumika. Tulipotaka Mwesigwa aelezee alimaanisha nini, alikanusha kuweza kusema maneno hayo.

Kifo cha Monic kinafanana sana na cha Kayla Birungi, mwanamke mwingine kutoka Uganda aliyekuwa akiishi katika eneo lile lile, na alifariki mwaka 2021 baada ya kuruka kutoka juu ya jengo ya makazi mjini Dubai ambalo tuna ushahidi linaendeshwa na Charles Mwesigwa.

Nambari ya simu ya mwenye nyumba, iliyoshirikiwa nami na familia ya Kayla, ilibainika kuwa ni mojawapo ya nambari za Mwesigwa.

Troy pia anathibitisha kuwa nyumba hiyo ilikuwa chini ya uangalizi wake, kama wanawake wengine wanne tuliowahoji kwa ajili ya uchunguzi huu.

Mwanamke mchanga aliyevaa kofia na glasi nyeusi na nywele nyeusi zilizonyooka anatabasamu kwa kamera

Chanzo cha picha, Instagram

Familia za Kayla wanasema kama ile ya Monic, kwamba walisikia kifo chake kilihusishwa na pombe na dawa za kulevya.

Lakini ripoti ya kiwango cha kusumisha ambayo BBC imeipata inaonyesha hakukuwa na chembechembe zozote katika mwili wake wakati wa kifo.

Wakati familia ya Kayla ilipafanikiwa kurejesha mwili wake Uganda na kumzika, mwili wa Monic haukuletwa nyumbani kupata maziko.

Uchunguzi wetu uligundua alizikwa kwa kaburi sehemu ya Makaburi ya Al Qusais Dubai inayoitwa “The Unknown”.

Inajumuisha makaburi mengi yasiyo na alama, ambayo mara nyingi hufikiriwa kuwa ya wafanyakazi wageni ambao familia zao hawakuwa na uwezo wa kusafirisha miili yao nyumbani.

Monic na Kayla walikuwa sehemu ya mtandao mkubwa wa watu kutoka Uganda waliokuwa wakihamia kwenda Mashariki ya Kati.

Uganda ikiwa inakabiliana na ongezeko la ukosefu wa ajira kwa vijana, kusafiri kufanya kazi nje – hasa katika nchi za Ghuba – imekuwa sekta kubwa inayochangia dola bilioni 1.2 ya kodi kwa nchi kila mwaka.

Lakini fursa hizi zinaweza kuwa na hatari.

Mariam Mwiza, mwanaharakati wa Uganda dhidi ya unyanyasaji, anasema amesaidia kuokoa zaidi ya watu 700 kutoka Ghuba.

“Tunapata kesi za watu ambao wameahidiwa kufanya kazi, tuseme, katika duka kubwa. Kisha [mtu huyo] anaishia kuuzwa kama kahaba,” alituambia.

Watu wanne wa familia ya Monic akiwemo mama yake walishikilia picha za Monic zilizoandaliwa

Kwa familia ya Monic, uchungu sasa umechanganyika na hofu. Hofu kwa familia nyingine ambazo zinaweza kupata hasara kama ile wanayoishi wao, ikiwa hakuna hatua itakayochukuliwa.

“Sote tunaangalia kifo cha Monica,” jamaa yake Michael alituambia. “Lakini ni nani kwa wasichana ambao bado wako hai? Bado wapo. Wanaendelea kutumbukia.”

BBC ilimuomba Charles “Abbey” Mwesigwa ajibu mashtaka yote yaliyotolewa katika uchunguzi wetu. Aliyanukuu yote kuwa ni ya uongo.

Alisema: “Haya yote ni mashtaka ya uongo.

“Nimesema mimi ni mtu wa sherehe tu, ninayewaita watu matajiri kujivinjari, ndiyo maana wasichana wengi wanasogea. Hiyo inanifanya nifahamu wasichana wengi hakuna zaidi ya hilo.”

Alisema pia: “[Monic] alikufa akiwa na pasipoti yake, maana hakuna mtu aliyekuwa anatakiwa kulipwa kwa ajili ya kumchukua. Kabla ya kifo chake, sikuweza kumuona kwa zaidi ya wiki nne hadi tano.

“Nilijua [Monic na Kayla] na [walikuwa] wakikodi na wamiliki tofauti wa nyumba. Ikiwa hakuna mtu katika nyumba hizo aliekamatwa au mwenye nyumba yoyote, basi kulikuwa na sababu. Matukio yote yalichunguzwa na polisi wa Dubai na labda wanaweza kuwasaidia.”

BBC ilimpigia simu kituo cha polisi cha Al Barsha kuomba kuona faili za kesi za Monic Karungi na Kayla Birungi.

Hawakujibu ombi hilo wala mashtaka ya kwamba vifo vya Monic na Kayla havikuchunguzwa vizuri.

BBC haikuweza kuona ripoti zozote za kiwango cha kusumisha juu ya Monic Karungi, au kuongea na mwenye nyumba wa nyumba alikokuwa Monic akiishi wakati wa kifo chake.

  • Ikiwa una maelezo yoyote ya kuongeza kwenye uchunguzi huu tafadhali wasiliana runako@bbc.co.uk
  • Maelezo ya mashirika yanayotoa taarifa kuhusu au usaidizi baada ya unyanyasaji wa kijinsia au kwa hisia za kukata tamaa yanapatikana bbc.co.uk/actionline.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *