Hata hivyo Israel imeendelea kusema operesheni zake za kijeshi huko Gaza zinalenga kuwaokoa mateka wote wanaozuiliwa na Hamas na kuliangamiza kabisa kundi hilo.

Matamshi ya Hamad Al-Thani yamekuja leo wakati viongozi wa mataifa ya Kiarabu na Kiislamu wakikusanyana mjini Doha kujadili shambulizi la Israel dhidi ya wanamgambo wa Hamas nchini Qatar.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Umoja wa Nchi za Kiarabu, Ahmed Aboul Gheit, amesema ni muda sasa wa dunia kuvunja ukimya wake kuhusu tabia ya Israel aliyoiita ya kitapeli.

“Miaka miwili ya ukimya juu ya uhalifu na ukatili unaofanyika Gaza inatoa picha kwa viongozi wanyakuzi  kwamba chochote kinawezekana na uhalifu unaweza kufanywa bila kuadhibiwa. wameendelea kuharibu nchi moja baada ya nyengine na kuleta vurugu katika eneo zima. Tunatoa ujumbe kwa jumuiya ya kimataifa kwamba ukimya umetosha kwa taifa hili la Israel lililochoma eneo zima la Mashariki ya Kati, lililosababisha njaa, mauaji na kuwakosesha watu makaazi bila kuwajibishwa.”

Viongozi hao wa kiarabu wanatumai kuja na majibu ya pamoja ya kuizuwia Israel kuendeleza kile walichosema ni uhalifu dhidi ya binaadamu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *