Wabunge nchini Chad, Jumatatu ya wiki hii walipitisha marekebisho ya katiba yanayoongeza muda wa rais kukaa madarakani kutoka miaka 5 hadi 7 na kwa kipindi kisichokuwa na ukomo.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Muswada huo uliwasilishwa na muungano wa chama tawala cha Patriotic Salvation Movement, ukifanyia marekebisho baadhi ya vipengele vya katiba iliyopitishwa mwezi Desemba mwaka 2023, ambapo wabunge 171 waliunga mkono.
Kinachofuata kwa sasa ni kwa muswada huo kupelekwa kwenye bunge la seneti kwa ajili ya wabunge kupiga kura kuthibitisha rasmi marekebisho hayo.

Kwa mujibu wa vipengele vilivyorekebishwa, sasa vitaruhusu rais kuchaguliwa kwa muda usiokuwa na kikomo kwa vipindi vya miaka 7, tofauti na sasa ambapo ilikuwa ni miaka mitano na ukomo wa kuhudumu kwa mihula miwili pekee.
Marekebisho haya pia yanatoa nafasi ya kuundwa kwa nafasi ya naibu waziri mkuu pamoja na kuongeza muda wa wabunge kuhudumu kutoka miaka 5 hadi 6, huku pia ukiondoa kinga ya kutoshtakiwa kwa maofisa wa serikali.