
Kundi la waasi wa AFC/M23 limezindua kikosi kipya cha zaidi ya wanajeshi 7,000 tarehe 14 Septemba Mashariki mwa DRC, wakati wa hafla iliyofanyika katika kituo chake cha mafunzo huko Rumangabo, katika eneo la Rutshuru, kaskazini mwa Goma. Akiwahutubia wanajeshi hao, mratibu wa vuguvugu hilo, Corneille Nangaa, alitoa hotuba kali na ya ushindi, licha ya mazungumzo ambayo yamepiga hatua mwishoni mwa juma lililiopita mjini Doha.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Kulingana na AFC/M23, wengi wa wanajeshi hawa 7,000 ni wanajeshi wa zamani wa FARDC, jeshi la Kongo, ambao walijisalimisha wakati wa kutekwa kwa mji wa Goma na kisha mji wa Bukavu, mashariki mwa DRC, pamoja na Wazalendo wa zamani na wanajeshi wapya.
Video ya sherehe za kufunga mafunzo yao, iliyosambazwa sana kwenye mitandao ya kijamii, inamuonyesha Corneille Nangaa, mratibu wa vuguvugu hilo, akiwataka wanajeshi wake kuendelea “kuikomboa” Kongo hadi Kinshasa. Pia anawataka “kudhibiti maovu yanayoikumba DRC” na kuahidi kwamba hivi karibuni wataunganishwa na wapiganaji wengine “12,000” katika mafunzo. Takwimu hii haijathibitishwa na chanzo chochote cha kujitegemea.
Maneno ya kawaida ya vita
Wakati Corneille Nangaa amezoea aina hii ya matamshi ya kivita, maonyesho hayo katika muktadha wa sasa yananuiwa kuonyesha nguvu, licha ya mazungumzo ambayo yamepiga hatua ndogo mwishoni mwa juma lililopita mjini Doha, Qatar, kuhusu suala la wafungwa.
Kuhusiana na Kinshasa, vyanzo pia vinaripoti kutumwa kwa wanajeshi wengi katika mstari wa mbele, haswa karibu na Uvira, ambapo kuwasili kwa wanajeshi na vifaa vya ziada kumeripotiwa, kutoka upande wa FARDC na Burundi.