
Kadhia ya mfumuko wa bei na upungufu mkubwa wa nishati ya mafuta vinatajwa kuwa masuala muhimu yanayowashughulisha zaidi wapigakura.
Wagombea wengine 15 akiwemo rais wa zamani Joyce Banda pia wanawania kiti cha urais lakini inatazamiwa kwamba mchukuano mkali utakuwa baina ya Rais Chakwera na Peter Mutharika.
Rais Chakwera aliingia madarakani mwaka 2020 akiituhumu serikali ya mtangulizi wake Mutharika kwa ufisadi wa kutisha.
Hata hivyo utawala wake nao umekumbwa na kashfa kadhaa za rushwa na kuuporomosha uchumi wa taifa hilo la kusini mwa Afrika.
Mbali ya uchaguzi wa rais, wapigakura wapatao milioni 22 watawachagua pia wabunge na madiwani.