
Mwito huo umetolewa kupitia tamko la pamoja la viongozi wa karibu mataifa 60 wanachama wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu na ile ya nchi za kiislamu baada ya kumalizika kwa mkutano wao wa dharura uliofanyika jana mjini Doha.
Viongozi hao wamesema mbali ya kutafakari upya mahusiano ya kidiplomasia na Israel, mataifa yote wanachama yanapaswa kuchukua hatua za kisheria na kiutendaji kuizuia Israel kuendelea na hujuma dhidi ya Wapalestina.
Mashambulizi ya Israel ya mjini Doha yamelemaza juhudi za kidiplomasia zilizokuwa zikiongozwa na Qatar na Misri kujaribu kumaliza vita vya karibu miaka miwili kwenye Ukanda wa Gaza.