
Raia wa Malawi, hivi leo wanapiga kura katika uchaguzi mkuu wa rais, Wabunge na madiwani, uchaguzi ambao unatarajiwa kuamua mustakabali wa taifa hilo kuhusu uchumi na vita dhidi ya rushwa.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Upinzani unatarajiwa kuwa kati ya rais wa sasa mchungaji Lazarus Chakwera na aliyekuwa rais wa nchi hiyo, Peter Mutharika.
Wagombea 17 wanatafuta uongozi wa nchi hiyo ya Kusini mwa Afrika, katika uchaguzi ambao wachambuzi wa siasa wanaona kuwa rais Chakwera anakabiliwa na ushindani mkali kutoka kwa mtangulizi wake, Peter Mutharika.
Hii itakuwa ni mara ya tatu kwa Chakwera na Mutharika kupambana, kwenye kinyanganyiro cha kutafuta urais.
Utawala wa Chakwera, umekumbwa na changamoto nyingi za kiuchumi na athari nyingi za mabadiliko ya tabia nchi hasa mafuriko lakini amekuwa akioùba kura, akiahidi kumalizia yale aliyoanzisha kama ujenzi wa barabara shule na hospitali.
Hata hivyo, Mutharu kwenye umri wa miaka 85, kampeni zake zimekuwa zikijitika kwenye ahadi ya kufufua uchumi na kurejesha uongozi ambao anasema, umeyumba.
Hata hivyo, uwepo wa Dalitso Kabambe, aliyekuwa Gavana wa Benki kuu, anayetafuta uongozi wa nchi hiyo, unaelezwa huenda ukatatiza ushindi wa mzunguko wa kwanza, Septemba 16 na kupeleka uchaguzi huo kwenda kwenye mzunguko wa pili.