Nchini Sudan, Jimbo la Kordofan Magharibi limekuwa likikumbwa na mapigano makali kwa wiki kadhaa kati ya jeshi na Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF). Katika kukabiliana na kusonga mbele kwa jeshi, ambalo wiki iliyopita liliteka mji wa kimkakati wa Bara, ulioko kwenye barabara inayounganisha El Facher, mji mkuu wa Darfur Kaskazini, na Khartoum, RSF ililenga ngome za jeshi na miundombinu kusini mwa nchi mnamo Septemba 14.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

RSF, ambayo imekuwa ikipambana na jeshi nchini Sudan kwa miezi 29, ilitumia ndege zisizo na rubani kulenga makao makuu ya Kitengo cha 18 cha jeshi pamoja na maeneo ya kimkakati ya kiraia kama vile ghala za mafuta kwenye Mto Nile na mji wa Kosti. Maeneo yote hayo yanapatikana katika Jimbo la White Nile, kusini mashariki mwa nchi. Kiwanda kikubwa zaidi cha umeme nchini Sudan huko Kosti kililengwa, kama vile uwanja wa ndege wa Kenana na uwanja wa ndege katika mji huo.

Siku ya Jumamosi ya wiki iliyopita, mji wa el-Obeid, mji mkuu wa Kordofan Kaskazini, ulikumba na mashambulizi ya anga yaliyotekelezwa na ndege zisizo na rubani za RSF, ingawa uko chini ya udhibiti wa jeshi. Jiji hili linakumbwa na mashambulizi ya anga mara kwa mara.

Mashambulizi ya droni za RSF

Siku chache zilizopita, mara tu baada ya kuanguka kwa mji wa kimkakati wa Bara, RSF ilidai kuhusika na mashambulizi ya ndege zisizo na rubani kwenye miundombinu na mitambo ya kijeshi huko Khartoum. Kituo cha umeme kililengwa, pamoja na kiwanda cha kusafisha mafuta. Mapigano makali yanaendelea karibu na el-Obeid, ambapo miji kama Kazkil na Rayache iko kila mara chini ya udhibiti kutoka kambi ya RSF kwenda kambi ya jeshi.

Juhudi za kufikia usitishaji mapigano kati ya pande zinazozozana hadi sasa hazijafaulu. Siku ya Jumamosi, Septemba 13, serikali ya Sudan ilikataa pendekezo la kusitisha mapigano la miezi mitatu kutoka kwa Quartet ya Sudan inayoongozwa na Marekani. Pande zote mbili zinasema zinataka kuendelea kupigana hadi ushindi kamili wa kijeshi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *