Upinzani nchini Sudan Kusini, umetoa wito wa uhamasishaji kwa wafuasi na vikosi vyake kujitayarisha kufanya mabadiliko ya uongozi wa serkali, ili kujibu mpango wa serikali wa kutaka kumfungulia kiongozi wake Riek Machar, mashtaka ya uhaini.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Kupitia taarifa kaimu mwenyekiti wa chama cha upinzani, Oyet Nathaniel Pierino, amewataka wafuasi na kitengo cha jeshi la upinzani kujitayarisha kupigania mabadiliko  ya serikali, Oyet akidai kwamba, serikali ya rais Salva Kiiri inatawala kwa mkono wa chuma, na hilo sharti likomeshwe.

Juma lililopita makamo wa Kwanza wa rais Riek Machar, alifunguliwa mashtaka ya uhaini, uhalifu wa vita na mauwaji na kuondolewa wadhifa wa makamo wa Kwanza wa rais, hii ni licha ya kuendelea kuzuiliwa nyumbani kwa muda sasa.

Kesi dhidi ya Machar inatokana na wapiganaji wa White Army kuvamia kambi ya kijeshi na kuwaua zaidi ya wanajeshi 250, Machar akitumiwa kuhusika kwani wapiganaji hao wanatoka katika kabila lake la  Nuer, tuhuma ambazo Machar na washirka wake wamekanusha vikali.

Ushirikiano kati ya rais Salva Kiiri na hasimu wake wa jadi wa kisiasa dkt Reik Machar unatishia kulitumbukiza tena taifa hilo kwenye vita vingine vya wenyewe kwa wenyewe, ambavyo tayari vimewahi sababisha vifo vya watu laki 400 miaka ya awali.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *