Tabaka hilo hutoa kinga kwa uso wa dunia dhidi ya miale ya jua na kutengamaa kwake kunatokana na miongo minne ya juhudi za kimataifa za kupunguza utoaji gesi chafuzi.

Ripoti hiyo ya Shirika la Hali ya Hewa la Umoja wa Mataifa, WMO, inasema tundu lililojitokeza kwenye tabaka la ozoni limeanza kupungua ukubwa na kuna matumaini kwamba litapotea kabisa mnamo miongo inayokuja.

Miaka 40 iliyopita wanasayansi waliarifu kwa mara ya kwanza kuhusu kitisho cha kuharibika kwa tabaka la ozoni na kuonya juu ya taathira zake kwenye uso wa dunia ikiwemo ongezeko la kiwango cha joto.

Tangu wakati huo mataifa ulimwenguni yalichukua hatua za kupunguza uzalishaji na matumizi ya vifaa vyenye mifumo inayotoa gesi chafuzi kama majokofu na viyoyozi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *