Hayo yameelezwa na shirika moja la kiraia nchini humo ambalo limearifu kwamba mashambulizi hayo yalitokea kati ya Septemba 11 na 12 kwenye maeneo ya kaskazini mwa mji mkuu, Port-au-Prince.

Shirika hilo liitwalo Mtandao wa Kitaifa wa Utetezi wa Haki za Binadamu, limesema hadi mwanzoni mwa wiki hii baadhi ya waathiriwa bado hawajapatikana na miili ya wale waliouawa bado iko vichakani ikiliwa na wanyama.

Mauaji hayo yanaonesha jinsi taifa hilo la kanda ya Karibia linavyoendelea kukumbwa na matatizo ya ukosefu wa usalama kutokana na kushamiri kwa makundi ya wahuni wanaobeba silaha.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *