Mashambulizi ya Israel yamegharimu maisha ya watu wasiopunguwa 14 usiku wa Ijumaa kuamkia Jumamosi katika Jiji la Gaza, maafisa wa eneo hilo wameripoti. Israel imezidisha mashambulizi yake katika siku za hivi karibuni na kuwataka Wapalestina kuuhama mji huo.
