#HABARI: Kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu imesogezwa mbele hadi Oktoba 6, 2025 baada ya usikilizwaji wa awali na upande wa utetezi kutaja orodha ya mashahidi wake.
Kesi hiyo imeahirishwa leo Jumatatu, Septemba 22, 2025 Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Dar es Salaam mbele ya kiongozi wa jopo la majaji, Jaji Dunstan Ndunguru baada ya upande wa mashtaka kuomba kuahirishwa kwa shauri hilo ili kupata muda wa kuwaandaa na kuwafikisha mashahidi wao mahakamani hapo, ombi ambalo limekubaliwa na Mahakama na kupanga kuendelea tena Oktoba 6, 2025.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania
(Feed generated with FetchRSS)