Wakati Uingereza, Australia, na Canada zimelitambua rasmi Taifa la Palestina siku ya Jumapili, na nchi nyingine za Magharibi, ikiwa ni pamoja na Ufaransa, zitafanya hivyo Septemba 22, nchi 52 kati ya 54 za bara la Afrika tayari zimetoa tamko hili la mfano, nyingi ya hizo tangu kutangazwa rasmi kwa taifa hili miaka 37 iliyopita. Nchi mbili ambazo ni Cameroon na Eritrea ndizo hazijalitambua taifa la Palestina.
Palestina, nchi ambayo tayari inatambuliwa na nchi 52 kati ya 54 za bara la Afrika