Riek Machar atafikishwa mahakamani leo Jumatatu, Septemba 22, pamoja na washtakiwa wenzake saba, wanachama wa chama chake cha upinzani, SPLM-IO, akiwemo Waziri wa Mafuta, Puot Kang, ambaye pia alisimamishwa kazi. Wanatuhumiwa kuanzisha mashambulizi dhidi ya jeshi la Sudan Kusini huko Nasir, Upper Nile, kaskazini mashariki mwa nchi hiyo, mwezi uliopita wa Machi.
Sudan Kusini: Kesi ya Riek Machar kuanza kusikilizwa Juba