ll
Maelezo ya picha, Mratibu wa mtandao Alina Juk (kushoto), aliyenaswa na kamera yetu ya siri, akisikiliza maagizo kuhusu kampeni ya kutoa taarifa potofu.

    • Author, Oana Marocico, Seamus Mirodan & Rowan Ings
    • Nafasi, BBC

Mtandao wa siri unaofadhiliwa na Urusi unajaribu kuvuruga uchaguzi ujao wa kidemokrasia katika eneo la Ulaya mashariki, BBC imegundua.

Kwa kutumia ripota wa siri, tuligundua mtandao huo uliahidi kuwalipa washiriki iwapo watachapisha propaganda zinazoiunga mkono Urusi na habari za uongo za kuhujumu chama tawala cha Moldova kinachounga mkono Umoja wa Ulaya kabla ya kura ya bunge ya Septemba 28 nchini humo.

Washiriki walilipwa ili kutafuta wafuasi kwa siri wa upinzani wa Moldova wanaounga mkono Urusi – na pia kufanya kile kinachojulikana kama kura ya maoni. Hili lilifanyika chini ya jina la shirika lisilokuwepo. Matokeo ya ya kura ya maoni, kwa mujibu wa mratibu yanaweza kuweka msingi wa kuhoji matokeo ya uchaguzi.

Matokeo ya kile kinachoitwa kura ya maoni, yanayopendekeza chama tawala kitashindwa, tayari yamechapishwa mtandaoni.



Source link

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *