Chanzo cha picha, Getty Images
China
imewahamisha maelfu ya watu na kuamuru takriban miji 10 kufunga shule na baadhi
ya biashara huku kimbunga kikali zaidi kwa mwaka kikitarajiwa katika pwani yake
ya kusini.
Kimbunga
hicho kinatarajiwa kupiga katika mkoa wa Guangdong nchini China siku ya
Jumatano, ambapo takriban watu 370,000 wamehamishwa hadi sasa, huku mamlaka
ikionya hali itakuwa mbaya.
Kimbunga Ragasa
kimepewa jina la “Mfalme wa Vimbunga” na shirika la hali ya hewa la
China na kinatarajiwa kuelekea kaskazini mwa Vietnam katika siku zijazo, na kinaweza
kuathiri mamilioni ya watu.
Siku ya
Jumanne, rafu za maduka makubwa huko Hong Kong zilikuwa tupu watu wakinunua
mkate, mboga mboga, nyama na tambi za papo hapo huku wakazi wakijiandaa.
Uwanja wa
Ndege wa Kimataifa wa Hong Kong ulisema unatarajia “idadi kubwa ya safariza
ndege” kuanzia siku ya Jumanne hadi siku inayofuata.
Katika miji
ya kusini mwa China, wamiliki wa maduka walirundika mifuko ya mchanga mbele ya
maduka yao ili kujiandaa na kuwasili kwa kimbunga, huku wakaazi katika maeneo
ya mabondeni karibu na mbele ya bahari wakiwa na wasiwasi haswa juu ya mawimbi
ya maji.
Wengi pia
wamefunga madirisha ya nyumba na biashara zao, wakitumaini kuzuia uharibifu kutokana
na upepo.
Bado
haijabainika ni kwa kiasi gani mabadiliko ya tabia nchi yamechangia kimbunga
cha Ragasa. Lakini joto linaloongezeka duniani linatarajiwa kuongeza dhoruba
na vimbunga kuwa vikali zaidi, kulingana na wanasayansi wa Umoja wa Mataifa.
Hiyo uwepo
wa upepo mkali, mvua kubwa na hatari ya mafuriko katika maeneo ya pwani.
Kimbunga Ragasa
kilipita katika kisiwa cha Taiwan usiku wa jana, takriban watu sita
walijeruhiwa na zaidi ya safari 100 za ndege za kimataifa kufutwa.
Ragasa kilipita
katika kisiwa cha mbali kaskazini mwa Ufilipino siku ya Jumatatu, na kuua mtu
mmoja huku maelfu ya familia zikihamishwa kabla ya kimbunga hicho kuanguka.
Shule na
ofisi za serikali zilifungwa, ikiwa ni pamoja na katika mji mkuu wa Manila.
Kimbunga Ragasa
kinavuma kwa upepo mkali wa hadi kilomita 285 kwa saa (177mph) katika kiwango
chake cha juu siku ya Jumatatu, na kimesababisha mafuriko, mawimbi ya dhoruba
na maporomoko ya ardhi katika nchi hiyo.
Kimbunga
kikuu cha Mangkhut cha 2018 – ambacho ndio kikubwa kikali zaidi kupiga eneo Hink Kong – kilijeruhi watu 200, kuzamisha meli na miundombinu kuharibika, na kuacha
hasira ya HK $ 4.6bn ($592m: £438m).
Mnamo mwaka
wa 2017, kimbunga Hato kilisababisha mafuriko makubwa na kujeruhi zaidi ya watu
100 katika jiji hilo.