Rais wa Malawi Lazarus Chakwera amekubali kushindwa katika uchaguzi mkuu uliofanyika wiki iliyopita, akisema katika hotuba yake ya leo kwa taifa kwamba ni wazi kuwa mpinzani wake Peter Mutharika amepata ushindi halali.

Rais Chakwera alichukua utawala nchini Malawi katika uchaguzi wa 2020 wakati alipomshinda rais wa wakati huo Mutharika wa chama cha  Democratic Progressive Party, DPP na ambaye anarudi tena katika kiti hicho baada ya miaka mitano.

Kampeni za uchaguzi huo zilitawaliwa na hali mbaya ya uchumi wa nchi hiyo ndogo ya kusini mwa Afrika, huku wakosoaji wakimshutumu Chakwera kwa usimamizi mbovu, kushindwa kukabiliana na ufisadi na kushindwa kutekeleza ahadi za kutengeneza ajira kwa vijana.

Kuelekea katika siku zake za mwisho ofisini, Chakwera ameahidi kufanikisha mchakato wa kukabidhi madaraka kwa Peter Mutharika kwa amani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *