Chanzo cha picha, Getty Images
Crystal Palace imeiambia Liverpool kuwa haina nia ya kumuuza kiungo wa kati wa England Adam Wharton, 21, katika dirisha la uhamisho la Januari. (Team talk)
Liverpool inajiandaa kumpa kiungo wa kati wa Uholanzi Ryan Gravenberch, 23, mkataba mpya wa muda mrefu. (Team talk)
Arsenal ina nia ya kumsajili winga wa Japan Takefusa Kubo mwenye umri wa miaka 24 kutoka Real Sociedad wakati wa uhamishowa wa wachezaji mwezi Januari mwakani. (Fichajes – kwa Kihispania)
Barcelona wamefikia makubaliano na Mholanzi Frenkie de Jong, 28, baada ya kiungo huyo ukubali kuongeza muda wake hadi 2029 kwa kupunguzwa mshahara. (Mundo Deportivo – kwa Kihispania)
Getafe inakaribia kumsajili mshambuliaji wa zamani wa Leeds United na Chelsea Patrick Bamford, 32, ambaye ni mchezaji huru baada ya kuondoka Leeds msimu wa kiangazi baada ya ya kuichezea klabu hiyo kwa miaka saba. (Football Espana)
Klabu za Arsenal na Liverpool zimefahamishwa kuwa winga wa Brazil Vinicius Junior mwenye umri wa miaka 25 hajui hatma yake ndani ya Real Madrid. (TBR Football)
Meneja wa Fulham Marco Silva anasema kiungo wa Wales Harry Wilson, 28, ambaye alifuatiliwa na Leeds msimu wa kiangazi, anatarajiwa kujadiliana na klabu hiyo kuhusu mpango wa kurefusha kandarasi yake. (Sky Sports)
Leeds inataka kuwasaini winga na kiungo mshambuliaji katika usajili wa Januari. (Football Insider)