
Mkutano ulioandaliwa na Rais wa Marekani Donald Trump kwa ajili ya kukutana na viongozi kadhaa wa Kiarabu na Kiislamu ulilenga kutafuta namna ya kumaliza vita katika Ukanda wa Gaza, hayo yameripotiwa na shirika la habari la Umoja wa Falme za Kiarabu leo Jumatano.
Mkutano huo umefanyika pembezoni mwa Mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa unaoendelea jijini New York, Marekani, na kuwahusisha viongozi wa mataifa kadhaa ikiwemo Jordan, Uturuki, Misri, Pakistan na Saudi Arabia.
Trump alisema mkutano huo ni hatua muhimu katika kutafuta suluhu ya mzozo wa Mashariki ya Kati.
“Nitafanya mkutano huu kuwa muhimu. Kwa hivyo huu utakuwa mkutano muhimu sana. Utakuwa mkutano na viongozi wakuu kutoka sehemu muhimu ya sayari yetu, Mashariki ya Kati. Na tunataka kumaliza vita huko Gaza. Tutavimaliza.”amesema Trump.,
Mkutano huo umefanyika huku kukiwa na wimbi la kuitambua Palestina kama nchi kutoka kwa nchi za Magharibi, hatua ambayo, hata hivyo, imekosolewa na Marekani.