
Ukraine imefanya shambulio la droni Jumatano katika mji wa kusini wa Urusi wa Novorossiisk na kuua watu wawili na kujeruhi wengine sita.
Mamlaka zimesema katika taarifa kupitia chaneli ya Telegram kwamba hali ya hatari imetangazwa katika mji huo ambao ni bandari kuu ya Urusi katika Bahari Nyeusi na wenye vituo muhimu vya usafirishaji wa mafuta na nafaka.
Mzozo huo umeendelea kuchukua sura mpya ambapo mapema leo Ikulu ya Urusi iliapa kuzidisha mashambulizi yake ya kijeshi nchini Ukraine na kuyatupilia mbali madai ya Rais wa Marekani Donald Trump kwamba nchi hiyo sasa haina uwezo.
Trump alisema kwamba Ukraine inao uwezo wa kuyarejesha maeneo yake yote yaliyochukuliwa na Urusi ambayo kulingana na kiongozi huyo, uchumi wake kwa sasa umedorora.