Wakati mfumuko wa bei ukipungua katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), hali ambayo inaweza kuashiria kuboreka kwa hali ya uchumi, mamlaka zina wasiwasi kuhusu ukubwa wa mishahara ya serikali. Ikichukuliwa kuwa juu sana ikilinganishwa na mapato ya kodi, suala la mishahara liko katikati ya mjadala, huku serikali ikijaribu kuiweka chini ya 5% ya Pato la Taifa.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 2 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

“Hatua za ujasiri zinahitajika ili kudhibiti suala hili, la sivyo kila kitu ambacho serikali inakusanya humezwa na mishahara, huku nchi ikihitaji kuwekeza katika miundombinu na kujitayarisha kwa siku zijazo,” ameonya Waziri wa Uchumi Mukoko Samba siku ya Jumanne. Suala laukubwa wa mishahara pia linasalia kuwa suala kuu la mjadala na washirika wa DRC, kama vile IMF na Benki ya Dunia.

Mwaka huu, baadhi ya sekta, kama vile ulinzi na usalama, zinakabiliwa na ongezeko fulani. Tangu mwezi wa Machi, mishahara ya wanajeshi na polisi imeongezwa maradufu. Bonasi ya mapigano pia imeanzishwa. Na bado haijaisha: kwa matarajio ya kuajiri wanajeshi wapya, mishahara ya jeshi inatarajiwa kukua kwa kasi zaidi kuliko ilivyotarajiwa.

Ili kudhibiti ongezeko hili, Ukaguzi wa Wanajeshi lazima uanzishe ukaguzi wa idadi ya wanajeshi, haswa katika maeneo ambayo hayajaathiriwa moja kwa moja na operesheni za kijeshi.

Lakini changamoto haiishii kwa jeshi. Juhudi kubwa tayari zimefanywa katika utumishi wa umma. Mnamo mwezi Juni 2023, serikali ilikuwa na wafanyakazi zaidi ya milioni 1.4; leo, kulingana na Wizara ya Utumishi wa Umma, kuna wafanyakazi 795,000, kufuatia mchakato wa urekebishaji.

Sera mpya ya mishahara inayokuja

Hata hivyo, kudhibiti idadi ya wafanyiakazi haitoshi. Mapema mwezi Septemba, Wizara za Bajeti na Utumishi wa Umma zilifanya kazi pamoja ili kuoanisha vipaumbele na kuandaa sera mpya ya mishahara. Hii inatarajiwa kabla ya mwisho wa mwaka.

Lengo lililotajwa liko wazi: kuweka ukubwa wa mishahara, inayokadiriwa kuwa 4.8% ya Pato la Taifa mnamo 2025, chini ya kiwango cha 5% katika muda wa kati. Kwa muda mrefu, mamlaka inalenga kupunguza uwiano huu kutoka 4.4% ya Pato la Taifa mwaka 2024 hadi karibu 4.1% ifikapo mwaka 2030.

Serikali inalenga kuimarisha ufufuaji wa uchumi, muda mfupi baada ya kutangaza kushuka kwa mfumuko wa bei. Kwa mara ya kwanza baada ya miaka minne, nchi hii inatarajiwa kumaliza mwaka kwa kiwango cha chini ya 10%. Kulingana na takwimu rasmi, inatarajiwa kufikia 7.8%. Hali hii inachukuliwa kuwa ya kuridhisha, pia inaendeshwa na kiwango cha ubadilishaji thabiti wa fedha.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *