
Rais wa Mamlaka ya Palestina Mahmoud Abbas ameuambia Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa siku ya Alhamisi kwamba mashambulizi ya Oktoba 7 “hayawakilishi raia wa Palestina,” akiikatisha tamaa Hamas kwa kuipa jukumu lolote katika utawala wa baadaye wa Palestina.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
“Tunapinga na kufutilia mbali kile Hamas ilitekeleza Oktoba 7,” tukio ambalo “haliwakilishi raia wa Palestina, wala mapambano yao ya haki ya uhuru na uhuru wa kujitawala,” amesema.
Wakati huo huo Kiongozi wa Mamlaka ya Palestina Mahmoud Abbas ameshtumu mauaji yanayofanywa na Israel katika Ukanda wa Gaza.
“Uhalifu dhidi ya ubinadamu” unaofanywa na Israel huko Gaza ni “moja ya sura za kutisha” za karne ya 20 na 21, Rais wa Palestina Mahmoud Abbas ametangaza katika hotuba ya video kwa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.
“Kinachofanywa na Israel sio uchokozi tu, ni uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu (…) ambao utarekodiwa katika kurasa za vitabu vya historia na katika dhamiri ya ubinadamu kama moja ya sura za kutisha zaidi za maafa ya kibinadamu ya karne ya 20 na 21,” ametangaza kiongozi huyo, ambaye alinyimwa visa na Marekani.