Kansela Merz amesema hayo jana Jumatano alipokuwa akilihutubia muungano wa tasnia ya kemikali na dawa mjini Berlin.

Amesema changamoto za mazingira ya sasa ya kimaeneo na kisiasa zinazoshuhudiwa sasa hujitokeza kwa nadra sana, na kuongeza kuwa anafanya kila juhudi “kurejesha” uhusiano na Marekani, hasa katika NATO na mahusiano ya kiuchumi.

Rais Donald Trump wa Marekani kwenye hotuba yake mbele ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa siku ya Jumanne, aliwadhihaki washirika wake wa NATO kwa kushindwa kuacha kununua mafuta ya Urusi, akiahidi kuliwekea vikwazo vikali taifa hilo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *