
Marekani inayompinga Abbas inaangazia ikiwa inalazimika kuizuia Israel kuunyakua Ukingo wa Magharibi.
Kiongozi huyo wa Palestina analihutubia Baraza hilo siku tatu baada ya Ufaransa kuongoza mkutano maalumu wa kilele, ambako mataifa kadhaa yalilitambua rasmi taifa la Palestina.
Serikali ya Rais Donald Trump inapinga kabisa utaifa wa Palestina na katika hatua ambayo haikutarajiwa ilimzuia Abbas na washauri wake waandamizi kwenda New York kuhudhuria mkutano huo. Lakini kusanyiko hilo lilipiga kura kwa wingi kumruhusu Abbas kuhutubia kwa njia ya video.
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ameapa kutoruhusu kuanzishwa kwa taifa la Palestina na mawaziri wake wanaoegemea mrengo wa kulia tayari wametishia kuunyakua Ukingo wa Magharibi ili kuondoa kabisa matarajio hayo ya uhuru kamili.