
Sarkozy, mwenye umri wa miaka 70, ameitaja hukumu hiyo kama “fedheha na dhuluma,” na kusisitiza atahakikisha analisafisha jina lake hadi mwisho wa maisha yake.
Mahakama ya Jinai ya Paris ilimkuta na hatia ya kushirikiana na mtandao wa kihalifu na kutoa hati ya kumkamata, ingawa haukutekelezwa mara moja.
Kwa mujibu wa uamuzi huo Sarkozy atalazimika kuanza kutumikia kifungo hata kama atakata rufaa.
Kisheria, wafungwa wenye umri wa miaka 70 na kuendelea wanaweza kuomba kupunguziwa adhabu.