Amesema hayo kwenye mahojiano ya kipindi cha Axios mjini New York mapema leo na kuongeza kuwa anatumai kupokea makombora ya masafa marefu kutoka Marekani ingawa hakuelezea zaidi.

Hata hivyo, rais huyo wa Ukraine ameondoa uwezekano wa kushambulia maeneo ya raia akisema wao sio magaidi.

Awali Naibu Mwenyekiti wa Baraza la Usalama la Urusi, Dmitry Medvedev, alimuonya vikali Zelensky kwa kauli yake ya kuishambulia Kremlin na ametishia kuushambulia tena mji mkuu wa Ukraine, Kiev.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *