
Kulingana na ripoti hiyo, visa hivyo vitaongezeka kutoka milioni 18.5 mwaka 2023 hadi milioni 30.5 mwaka 2050.
Watafiti wanasema hii inatokana na jamii kuwa na idadi kubwa ya wazee ambao ni wahanga wakubwa wa saratani na kuongeza kuwa karibu asilimia 42 ya vifo milioni 10.4 vya saratani mwaka 2023, vilitokana na sababu zinazoweza kubadilishwa.
Sababu hizo ni pamoja na matumizi ya tumbaku, yaliyosababisha asilimia 21.4 ya vifo vya saratani na katika nchi masikini, ngono isiyo salama ilichangia pakubwa, hasa kwa kuwa inaweza kusambaza virusi vya HPV vinavyosababisha saratani ya shingo ya kizazi.