Chanzo cha picha, Rex Features
Manchester United inamtaka mshambuliaji wa Uingereza Harry Kane, 32, ambaye huenda akaondoka Bayern Munich msimu ujao wa kiangazi. (Star)
Mkufunzi wa Tottenham Thomas Frank anasema Kane, mfungaji bora wa klabu hiyo, “anakaribishwa nyumbani,” kwa mikono miwili, lakini hatarajii mshambuliaji huyo kuondoka Ujerumani hivi karibuni. (Sky Sports)
Kiungo wa kati wa Uingereza Kobbie Mainoo, 20, yuko tayari kuondoka Manchester United mwezi Januari. Alikuwa na ombi la mkopo klabu nyingini kumsajili kwa lilikataliwa na United katika majira ya kiangazi. (Mirror)
Bayern Munich inafikiria kumpa mkataba mpya winga wa Ufaransa Michael Olise mwenye umri wa miaka 23 baada ya mchezaji huyo kuhusishwa na tetesi za kuhamia Liverpool. (Liverpool Echo)
Arsenal imewasiliana na mshambuliaji wa Uturuki Kenan Yildiz, 20, lakini Juventus, ambao walikataa ofa kutoka kwa Chelsea msimu wa kiangazi, wanakadiria thamani yake kuwa kati ya Euro milioni 80-100. (Tutto Juve via Goal)
Chelsea ina mpango wa kumsajili beki Mfaransa Ismael Doukoure, 22, ambaye kwa sasa yuko katika klabu inayomilikiwa na BlueCo ya Strasbourg, huku mchezaji huyo akiwaniwa na klabu kadhaa za Ligi ya Premia. (TBR Football)
Chanzo cha picha, Getty Images
Aston Villa wanapania kumsajili mshambuliajiwa Uingereza Jadon Sancho, 25, ambaye anachezea klabu hiyo kwa mkopo kutoka Manchester United. (National World)
Imetafsiriwa na Ambia Hirsi