
Rais wa zamani wa Ufaransa Nicolas Sarkozy, amepatikana na hatia ya kupanga njama kuhusu sakata la kufadhiliwa na serikali ya Libya, wakati wa kampeni za uchaguzi wa urais mwaka 2007.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Mahakama imetoa hukumu hiyo siyo ya Alhamisi, jijini Paris, mbele ya Sarkozy aliyekuwa Mahakamani, lakini Jaji, Nathalie Gavarino, amemfutia mashtaka mengine ya ufisadi, yaliyokuwa yanamkabili.
Jaji Gavarino, katika maamuzi yake, amesema Sarkozy, kwa kufahamu, aliwaruhusu washirika wake wa karibu, kufanya jitihada za kupata msaada wa fedha kutoka kwa serikali ya Libya, chini ya aliyekuwa kiongozi wa taifa hilo Muammar Kaddafi, aliyeuawa mwaka 2011.
Hukumu ya kifungo, inatarajiwa kutolewa baadaye, huku viongozi wa mashtaka wakipendkeza kuwa Sarkozy, afungwe jela miaka saba na atozwe faini ya 300,000.
Aidha, viongozi wa mashtaka wanataka washtakiwa wenzake 11, wafungwe jela kati ya mwaka mmoja hadi sita.