
Mwenyekiti wa Halmashauri Kuu ya umoja huo Mahmoud Ali Youssouf, ametuma salamu hizo hizo kupitia mtandao wa X akiwapongeza Wamalawi wote kwa kushiriki mchakato huo wa kidemokrasia kwa uaminifu, amani na utulivu.
Mutharika aliyekuwa madarakani kati ya mwaka 2014 hadi 2020 amechaguliwa tena kwa karibu asilimia 57 ya kura kuliongoza taifa hilo lenye watu milioni 21.
Mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi nchini humo, Annabel Ntalimanja baada ya kutangaza matokeo hayo amesema:
“Sisi sote ni Wamalawi na tuko imara zaidi ya vyote vinavyotutenganisha. Tushirikiane kuitumikia nchi yetu na kuviandalia vizazi vyetu vijavyo Malawi iliyo bora, imara na yenye mafanikio.”
Mutharika amempiku rais anayeondoka Lazarus Chakwera aliyepata asilimia 33, hii ikiwa ni kulingana na Tume hiyo ya uchaguzi jana Jumatano.