Haiti, iliyoharibiwa na ghasia za magenge, ni “nchi iliyo katika vita,” ametangaza Laurent Saint-Cyr, Rais wa Baraza la Rais la Mpito la Haiti, katika Umoja wa Mataifa siku ya Alhamisi, Septemba 25, kwa mara nyingine tena akitoa wito wa kuungwa mkono zaidi na jumuiya ya kimataifa.

Imechapishwa:

Dakika 2 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

“Kila siku, maisha ya watu wasio na hatia yanazimwa kwa risasi, moto, na hofu. Vitongoji vyote vinatoweka, na kulazimisha zaidi ya watu milioni moja kwenda uhamishoni na kuharibu kumbukumbu, uwekezaji, na miundombinu,” amesema Rais wa Baraza la Rais la Mpito la Haiti.

“Maelfu ya vijana wanahukumiwa kukata tamaa; mamia ya wasichana na wanawake waliobakwa hubeba makovu ya unyanyasaji milele katika miili na roho zao […]. Hospitali zinaharibiwa, kuchomwa moto, au kulazimishwa kufunga milango yao.” “Madaktari wakimbia, watu wanafariki kwa kukosa huduma,” amebainisha Laurent Saint-Cyr.

“Hii ndio taswira ya Haiti leo: nchi iliyo vitani, Guernica ya kisasa, janga la kibinadamu kwenye mlango wa Marekani, safari ya saa nne tu kutoka hapa!” Ameshangaa.

Kikosi cha Kenya kilitumwa kwa matokeo tofauti

Katika kujaribu kuzuia unyanyasaji wa magenge yanayodhibiti karibu mji mkuu wote, Port-au-Prince, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa liliidhnisha mwaka 2023 kwa kuundwa kwa Misheni ya Kimataifa ya Usalama (MMAS), inayoongozwa na Kenya, kusaidia polisi wa Haiti waliozidiwa nguvu. Lakini kikosi hicho, ambacho hakina vifaa vya kutosha na kinachofadhiliwa kidogo, kimetuma wanajeshi elfu moja tu kati ya 2,500 wanaotarajiwa, na matokeo yake sasa si mazuri.

Katika muktadha huu, Marekani inashinikiza kuigeuza kuwa “kikosi cha kukandamiza magenge” cha zaidi ya askari 5,500 na wanajeshi. Mpango huu unaungwa mkono na Laurent Saint-Cyr, ambaye amebainisa siku ya Alhamisi hatari ya mzozo wa Haiti kuenea kanda nzima.

“Haiti inajikuta katika kitovu cha tishio la kikanda ambalo halijawahi kushuhudiwa. Mitandao ya uhalifu yenye nguvu na yenye silaha nyingi inatafuta kuyumbisha nchi na kutawala uchumi wa eneo letu lote la pamoja,” amesema.

“Ikiwa tutashindwa kukabiliana nao katika ardhi yetu, itakuwa ni udanganyifu kuwadhibiti mahali pengine katika kanda,” ameongeza, akitoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuonyesha “azma sawa” katika suala hili kama katika mapambano dhidi ya ugaidi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *