Chanzo cha picha, Getty Images
Liverpool ina mataumaini kuwa itafanikiwa kumshawishi mlinzi wa Ufaransa Ibrahima Konate, 26, kusaini kandarasi mpya huku klabu za Arsenal, Chelsea na Manchester City zikimuwania. (TBR Football)
Kiungo wa Barcelona na Uholanzi Frenkie de Jong, 28, analengwa na Manchester United. (Football Insider)
Klabu ya Bayern Munich inajiandaa kumpa kandarasi ya muda mrefu mshambuliaji wa Senegal Nicolas Jackson, 24, ambaye kwa sasa anaichezea kwa mkopo klabu hiyo ya Ujerumani kutoka Chelsea. (Bild – kwa Kijerumani – usajili unahitajika)
Manchester United imefikia mkataba na Fortaleza kumsaini kiungo wa kati wa Colombia Cristian Orozco mwenye umri wa miaka 17 mara atakapofikisha umri wa miaka 18 mwezi Julai. (Athletic)
United pia wanatazamia kukamilisha dili la mlinda lango wa Derby Muingereza Charlie Hardy, 16. (Sun)
Newcastle ni miongoni mwa vilabu vinavyofuatilia hali ya kiungo wa kati wa Ufaransa Eduardo Camavinga, 22, ambaye anafikiria kuondoka Real Madrid. (Football Insider)
Chanzo cha picha, Getty Images
Arsenal inatarajiwa kusaini mikataba miwili na klabu ya Real Sociedad ya thamani ya pauni milioni 75 kuwasajili wachezaji wake wawili ambao ni winga wa Japan Takefusa Kubo, 24, na mlinzi wa Ufaransa Lucien Agoume, 23. (Fichajes – kwa Kihispania)
Chelsea imejiondoa katika kinyang’anyiro cha kumsajili kipa wa Italia Gianluigi Donnarumma, 26, anayeichezea Manchester kwa mkopo. (Teamtalk)
Imetafsiriwa na Ambia Hirsi