Konate

Chanzo cha picha, Getty Images

Real Madrid wanafuatilia kandarasi ya mlinzi wa Liverpool na Ufaransa Ibrahima Konate, 26, kwa nia ya kumsajili kama mchezaji huru msimu ujao mkataba wake wa sasa utakapokamilika. (ESPN)

Beki wa Uingereza John Stones, 31, anatazamiwa kuanza mazungumzo na Manchester City kuhusu mkataba mpya na mkataba wake wa sasa unaotarajiwa kumalizika msimu wa joto. (Mirror)

Aston Villa wanafikiria kutoa ofa kwa mshambuliaji wa Sunderland mwenye umri wa miaka 25 Wilson Isidor mwezi Januari. (Football Insider)

Wilson Isidor

Chanzo cha picha, Getty Images

Crystal Palace wanatarajia Liverpool kurejea na ofa ya kumnunua beki wa Uingereza Marc Guehi, 25, mwezi Januari baada ya beki wa kati wa Italia Giovanni Leoni, 18, kuwekwa pembeni kwa mwaka mmoja kutokana na jeraha. (TBR Football)

Liverpool pia wanamfuatilia mlinzi wa Uruguay na Barcelona Ronald Araujo, 26, kama chaguo la beki wa kati. (Caught Offside)

Juventus wanataka kumuuza mchezaji anayelengwa na Manchester United na Chelsea Dusan Vlahovic, 25, mwezi Januari badala ya kumruhusu mshambuliaji huyo wa Serbia kuondoka bure msimu ujao wa joto. (Gazzetta dello Sport )

Dusan Vlahovic

Chanzo cha picha, Getty Images

Chelsea wanaangalia chaguo la mlinda lango huku wakipanga kumuuza mlinda lango wa Uhispania Robert Sanchez, 27, mwishoni mwa msimu huu. (Fichajes)

Kiungo wa kati wa Uingereza Morgan Rogers, 23, ameanza mazungumzo na Aston Villa kuhusu kandarasi mpya huku vilabu kadhaa vya Ligi ya primea vikiwa na nia ya kumnyakua. (Football Insider)

Nottingham Forest imetoa onyo kwa Manchester United, Tottenham, Newcastle na Liverpool huku kukiwa na nia ya kumnunua kiungo wa kati wa Uingereza Elliot Anderson, 22. (TBR Football)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *