Vikwazo vilidhoofisha uchumi wa Iran kabla ya kuondolewa chini ya makubaliano ya 2015

Chanzo cha picha, Reuters

Vikwazo vikubwa vya kiuchumi na kijeshi dhidi ya Iran
vilivyoondolewa chini ya makubaliano ya kihistoria ya kimataifa kuhusu mpango
wake wa nyuklia miaka 10 iliyopita vinatarajiwa kurejeshwa Jumamosi usiku
kuzuia mafanikio ya dakika za mwisho.

Haya yanajiri baada ya Uingereza, Ufaransa na Ujerumani
kuliandikia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa mwezi uliopita, na kuishutumu
Iran kwa kushindwa kutekeleza ahadi zake. Hilo lilizua utaratibu wa kuipa Iran
siku 30 kutafuta suluhu la kidiplomasia ili kuepusha vikwazo vilivyowekwa upya.

Iran imeitaja hatua hiyo kuwa kinyume cha sheria na inasema
kuwa itasimamisha ushirikiano na shirika la kimataifa la nyuklia la Wakala wa
Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) iwapo vikwazo vitarejeshwa.

Iran ilizidisha shughuli iliyopigwa marufuku ya nyuklia
baada ya Marekani kujiondoa katika makubaliano hayo mwaka 2016.

Unaweza kusoma;

  • Je, Marekani kuishambulia tena Iran?
  • Kwa nini Iran hairuhusiwi kuwa na silaha zake za nyuklia?
  • Je, Iran ilikuwa karibu kutengeneza silaha za nyuklia?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *