Chanzo cha picha, Getty Images
Liverpool na Manchester United wanatazamiwa kushindania usajili wa pauni milioni 65 wa mlinzi wa Everton mwenye umri wa miaka 23 wa Uingereza Jarrad Branthwaite. (Mirror)
Manchester United wanapanga kumnunua kiungo wa kati wa Atletico Madrid mwenye umri wa miaka 25 Conor Gallagher. (Express)
Chanzo cha picha, Getty Images
Barcelona wamefikia mafanikio makubwa kwa kiungo wa kati wa Uholanzi Frenkie de Jong, 28, ambaye amekubali kuongeza muda wake wa kukaa hadi 2029 kwa kupunguzwa mshahara. (Mundo Deportivo – in Spanish)
Liverpool wameambiwa hawana nafasi kabisa ya kuwashawishi Crystal Palace kuwauzia kiungo wa kati wa England Adam Wharton, 21, katika dirisha la uhamisho la Januari. (TeamTalk)
Chanzo cha picha, Getty Images
Atletico Madrid wanamtazama mshambuliaji wa Marseille Muingereza Mason Greenwood mwenye umri wa miaka 23, ambaye klabu hiyo ya Ufaransa ina thamani ya £65m. (Fichajes – in Spanish)
AC Milan wanavutiwa na beki wa Liverpool Joe Gomez mwenye umri wa miaka 28 na wanafikiria kuhama mwezi Januari. (Calciomercato – in Italian)
Chanzo cha picha, Getty Images
Liverpool wanachunguza uwezekano wa kumsajili beki wa Bayern Munich mwenye umri wa miaka 26 kutoka Ufaransa Dayot Upamecano kwa uhamisho wa bure msimu ujao. (Falk Christian)
Chelsea wanatumai kuipiku Real Madrid katika kuinasa saini ya kiungo wa kati wa Como na Argentina Nico Paz, 21. (Offside)
Chanzo cha picha, Getty Images
Meneja wa Benfica Jose Mourinho ana nia ya kumsajili mshambuliaji wa zamani wa Al-Ittihad mwenye umri wa miaka 37 Karim Benzema. (Marca in Spanish)
Tottenham inaweza kumrejesha winga Mwingereza Mikey Moore mwenye umri wa miaka 18 kutoka kwa mkopo katika klabu ya Rangers mwezi Januari. (Football Insider)
Chelsea wanapanga kumnunua kiungo wa kati wa Juventus wa Italia Manuel Locatelli, 27, lakini wanakabiliwa na ushindani kutoka kwa Newcastle, Aston Villa, West Ham na Bayer Leverkusen. (Offside)
Chanzo cha picha, Getty Images
Manchester United wanamfikiria Graham Potter baada ya kutimuliwa na West Ham kama mbadala wa kushtukiza iwapo Ruben Amorim ataondoka. (Fichajes – in Spanish)
Sunderland watafikiria kumuuza mlinzi wa Uingereza Dennis Cirkin mwenye umri wa miaka 23 mwezi Januari. Mkataba wake unamalizika msimu ujao. (TBR Football)