
Chanzo cha picha, Getty Images
Manchester United wana nia ya kumsajili mshambuliaji wa Juventus, raia wa Serbia, Dusan Vlahovic, 25, katika dirisha la uhamisho la Januari. (Gazzeta)
Kiungo wa kati wa Manchester City, raia wa Ureno, Bernardo Silva, 31, anafikiria kuhamia ligi ya Saudi Arabia mkataba wake utakapokamilika msimu ujao. (TalkSport)
Kiungo wa kati wa Ureno Joao Neves, 21, analengwa na Manchester City, lakini timu yake ya Paris St-Germain wanatarajiwa kukataa kumuuza. (Football Insider)
Liverpool huenda wakapigwa bei kubwa katika kumnunua mshambuliaji wa Atletico Madrid, raia wa Argentina, Julian Alvarez, 25, kwani timu hiyo ya La Liga inataka takribani pauni milioni 100. (Football Insider)

Chanzo cha picha, NDTV
Real Madrid inawafuatilia viungo wawili wa Chelsea – mchezaji wa kimataifa wa Argentina mwenye umri wa miaka 24 Enzo Fernandez na mchezaji wa kimataifa wa Ecuador mwenye umri wa miaka 23 Moises Caicedo. (TBR Football)
Aliyekuwa meneja wa timu ya taifa ya Uingereza Gareth Southgate yuko kwenye orodha ya watu watatu wanaotajwa kuwa meneja wa Manchester United, iwapo Ruben Amorim atatimuliwa. (Talksport)
AC Milan wameanza mazungumzo na mlinzi wa Uingereza Fikayo Tomori, 27, kuhusu mkataba mpya, huku klabu za Ligi Kuu ya England zikiwa na nia ya kumtaka. (Fabrizio Romano)
Leeds United inamfuatilia kiungo wa kati wa Brazil, Gustavo Prado, 20, huku timu yake ya Internacional ikiwa tayari kupokea ada ya takriban pauni milioni 17 (SportWitness via Correio do Povo)