.

Chanzo cha picha, Reuters

Rais wa
Marekani Donald Trump anatarajia kukamilisha pendekezo la mpango wa amani
wa Gaza katika mkutano wa Jumatatu na Waziri Mkuu wa Israel, Trump aliambia
Reuters siku ya Jumapili, wakati vifaru vya Israel vikisonga mbele zaidi katika
mji wa Gaza huku Hamas ikisema imepoteza mawasiliano na mateka wawili waliokuwa
wameshikiliwa huko.

Hatima ya
mateka hao wawili, waliosababisha hisia kali ndani ya Israel, inaweza kuwa na
athari mbaya kwenye mkutano kati ya Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu
na Trump siku ya Jumatatu.

Kikosi cha
kijeshi cha Hamas, Al-Qassam Brigedi, kiliitaka Israel siku ya Jumapili
kuwarudisha nyuma wanajeshi wake na kusitisha mashambulizi ya anga katika mji
wa Gaza kwa saa 24 ili wapiganaji waweze kuwapata mateka.

Trump
aliliambia shirika la habari la Reuters katika mahojiano ya simu kuwa amepokea “jibu la kutia moyo” kutoka kwa Israel na viongozi wa Kiarabu kuhusu
pendekezo la mpango wa amani wa Gaza na kwamba “kila mtu anataka makubaliano
yafikiwe.”

Hamas
ilisema bado haijapokea pendekezo lolote kutoka kwa Trump wala kutoka kwa
wapatanishi.

Israel
imefanya shambulio kubwa la ardhini katika mji wa Gaza, na kusambaratisha
wilaya nzima huku ikiamuru mamia kwa maelfu ya Wapalestina kukimbilia katika
kambi zilizo na mahema, katika kile Netanyahu anasema ni kutaka kuangamiza
Hamas.

Soma zaidi:

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *