k

Chanzo cha picha, AFP via Getty Images

Kufuatia makubaliano ya ulinzi kati ya Pakistan na Saudi Arabia, kuna mjadala unaoendelea kuhusu athari zake kwa eneo hilo na umuhimu wake katika siasa za kimataifa.

Pakistan na Saudi Arabia zina Mkataba wa Kimkakati wa Ulinzi wa Pamoja (SMIDA) unaohusu ushirikiano katika masuala ya ulinzi na usalama. Chini ya makubaliano haya, uvamizi dhidi ya nchi moja utazingatiwa kuwa uchokozi dhidi ya nchi zote mbili.

Kwa mujibu wa wachambuzi, kutangazwa kwa makubaliano ya pamoja ya ulinzi kati ya Saudi Arabia na Pakistan kumezua taharuki kwa sababu kadhaa.

Baadhi ya wachambuzi wana maoni kuwa makubaliano haya ya kimkakati yanaweza kusababisha mabadiliko makubwa ya kikanda na pia yanaweza kuathiri mkakati wa Israel juu ya na eneo hilo.

Wachambuzi wengi wanaamini hii ni hatua ya kwanza kubwa ya ulinzi kuchukuliwa na nchi yoyote ya Ghuba tangu shambulizi la Israel nchini Qatar Septemba 9.

Kwa mujibu wa wataalamu, mashambulizi hayo ya Israel yamezidisha hofu kwa nchi za Ghuba kwamba azma ya Marekani ya kuzilinda imedhoofika kwa kiasi fulani.

Mwanamfalme wa Saudia Mohammed bin Salman alielezea shambulio la Israel huko Doha kama ‘uchokozi wa kinyama.’

‘Tukio la ghafla na la kushangaza’

VC

Chanzo cha picha, Getty Images

Valenia Chakarova, mtafiti na mkurugenzi wa Taasisi ya Austria juu ya Ulaya na Sera za Usalama, anasema makubaliano kati ya Saudi Arabia na Pakistan ni maendeleo ya ghafla na ya kushangaza.

Kulingana naye, hii inaonyesha kuwa Saudi Arabia haijaridhishwa na utegemezi kwa Marekani juu ‘usalama wake.”

Chakarova aliandika kwenye mtandao wa kijamii wa ‘X’ kwamba kwa makubaliano haya Mashariki ya Kati na Asia Kusini zinaingia katika siasa mpya za kijiografia.

Wakati huo huo, katika mahojiano na BBC, mtafiti wa siasa wa Saudi Arabia Mubarak Al-Ati alisema, “makubaliano haya si ya kushangaza. Saudi Arabia na Pakistan zimekuwa na ushirikiano kwa miaka 80, na hilo linajulikana.”

Al Aati anaamini jambo muhimu katika makubaliano haya ni kwamba yamekuja wakati eneo hilo na jumuiya ya kimataifa vinapitia hali tata sana za kisiasa.

Kulingana na Wizara ya Ulinzi ya Saudia, makubaliano ya hayo yanalenga kuimarisha ushirikiano wa kiulinzi kati ya Saudi Arabia na Pakistan na ‘kuzuia’ kwa pamoja uchokozi wowote.

Pia inaeleza kuwa uchokozi wowote dhidi ya nchi yoyote ni uchokozi dhidi ya zote mbili.

Akizungumza na BBC, Mubarak al-Ati alidokeza makubaliano haya, yanatokana na kuongezeka kwa vitendo vya Israeli katika eneo hilo na usaliti wa mshirika wake wa kimkakati Marekani wakati wa shambulio la Israeli dhidi ya Qatar.”

Kwa miongo kadhaa, makubaliano yamekuwepo kati ya Marekani na nchi sita za Ghuba—Bahrain, Kuwait, Oman, Qatar, Falme za Kiarabu, na Saudi Arabia—ambapo Marekani inazihakikishia usalama nchi hizo sita ili kupata mafuta na gesi.

Kwa mujibu wa jarida la Uingereza la The Economist, nyufa za kwanza katika makubaliano haya zilionekana wakati waasi wa Houthi wanaoungwa mkono na Iran walipoishambulia Saudi Arabia mwaka 2019 na Umoja wa Falme za Kiarabu mwaka 2022. Katika matukio yote mawili, hakuna hatua muhimu iliyochukuliwa na Marekani.

Akizungumza na BBC, mchambuzi wa Saudia, Al Aati anasema nchi yake “haitaki kutegemea mshirika mmoja kwa matatizo yake ya kiusalama au ya kimkakati. Kwa hivyo, inaona ni muhimu kubadilisha washirika wake.”

Wachambuzi wanaamini makubaliano hayo mapya yanaweza kusababisha hali ya mambo. Chini ya makubaliano haya, Pakistan inaweza kupeleka makombora yake au silaha zake zozote kwenye ardhi ya Saudia.

Pakistan na Saudia

o

Chanzo cha picha, GOP

Pakistan ndio nchi pekee yenye Waislamu wengi ambayo inamiliki silaha za nyuklia. Islamabad inamiliki zaidi ya silaha 170 za nyuklia na vichwa vyenye uwezo wa kubeba nyuklia.

Saudi Arabia pia imetangaza kuwa inafikiria kuongeza uwekezaji katika sekta mbalimbali nchini Pakistan hadi kufikia dola bilioni 25.

Kulingana na Bloomberg, Mfuko wa Maendeleo wa Saudi unatazamia kuwekeza mabilioni ya dola katika sekta ya madini na petroli nchini Pakistan.

Saudi Arabia pia inafikiria kuongeza amana zake na Benki Kuu ya Pakistan hadi dola bilioni mbili.

Kulingana na shirika la serikali la Saudi Press Agency (SPA), makubaliano mapya ya ulinzi na Pakistan yanajengwa juu ya karibu wa miongo minane ya ushirikiano wa kihistoria, udugu, na mshikamano wa Kiislamu.

Pia yanaakisi maslahi ya pamoja ya kimkakati na ushirikiano wa kiulinzi kati ya nchi hizo mbili.

Kwa mujibu wa wachambuzi, ahadi ya usalama ya kulinda misikiti miwili mitakatifu ya Mecca na Madina ndiyo ‘msingi wa mshikamano’ kati ya Pakistan na Saudi Arabia.

Kwa mara ya kwanza 1960, jeshi la Pakistan lilifika katika ardhi ya Saudi Arabia, wakati kukiwa na hofu ya vita vilivyoanzishwa na jeshi la Misri huko Yemen.

Baada ya hayo, Pakistan na Saudi Arabia zilizidisha ukaribu huku kukiwa na hofu ya mgogoro baada ya Mapinduzi ya Iran mwaka 1979.

Wakati wa uvamizi wa Iraq nchini Kuwait mwaka 1991, Pakistan pia ilituma kikosi cha kijeshi nchini Saudi Arabia, ambacho kilikabidhiwa jukumu la kulinda maeneo matakatifu ya Makka na Madina.

Mwaka 2016, Pakistan ilijiunga na muungano wa kijeshi wa nchi za Kiislamu unaoongozwa na Saudi Arabia kupambana na ugaidi.

Kufikia 2018, zaidi ya maafisa elfu moja wa Jeshi la Pakistani walikwenda Saudi Arabia kwa mafunzo.

Nchi za Ghuba zitajiunga?

K

Chanzo cha picha, Pakistan PM’s office

Baadhi ya wachambuzi wanaielezea Saudi Arabia kama ‘mfadhili wa kimya kimya’ wa mpango wa nyuklia wa Pakistan, akichangia bajeti ya ulinzi ya Pakistan na kupanua silaha zake za nyuklia.

Kwa mujibu wa Talha Abdur Razzaq, mtafiti wa masuala ya usalama wa Mashariki ya Kati katika Chuo Kikuu cha Exeter, makubaliano ya pamoja ya ulinzi kati ya Saudi Arabia na Pakistan yanaweza kuwa kiini cha mapatano ambayo yanaweza pia kujumuisha nchi nyingine katika eneo hilo.

Katika chapisho lake kwenye ‘X’, alisema nchi za eneo hilo hazichukulii tena dhamana ya usalama ya Marekani, kwa uzito na sasa nchi za Ghuba zinapitia mchakato wa kubadilisha makubaliano yao ya usalama.

Waziri wa Ulinzi wa Pakistan, Khawaja Asif, katika mahojiano na Al-Jazeera TV, alisema akijibu swali kuhusu ushiriki wa nchi nyingine za Ghuba, “inawezekana.”

“Ikiwa nchi yoyote ya GCC (Baraza la Ushirikiano la Ghuba) itatoa dalili kama hiyo, basi kwa vile tumefikia makubaliano ya pande zote na Saudi Arabia, tunaweza kufikiria kujumuisha nchi zingine pia.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *