.

Chanzo cha picha, EPA

Rais wa
Marekani Donald Trump na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu wanasema
wamekubaliana mpango mpya wa amani wa Gaza, na kuionya Hamas kuukubali.

Mpango huo
unapendekeza kusitishwa mara moja kwa operesheni za kijeshi na Hamas kuwaachilia
huru mateka 20 wa Israel na wengine zaidi ya 20 ambao wanaaminika kufariki
dunia ndani ya saa 72, ili kubadilishana na mamia ya raia wa Gaza wanaozuiliwa.

Chanzo cha
Palestina kinachofahamu mazungumzo ya kusitisha mapigano kiliambia BBC kwamba
maafisa wa Hamas wamepewa pendekezo lenye kugusia vipendele 20 la Ikulu ya Marekani.

Moja wapo ya
mapendekezo ni kwamba Hamas haitakuwa na jukumu lolote katika kutawala Gaza, na
kufungua mlango kwa upatikanaji kamili wa taifa la Palestina.

Akizungumza
katika mkutano na wanahabari kufuatia mazungumzo katika Ikulu ya White House,
Trump aliutaja mpango huo kuwa “siku ya kihistoria kwa amani”.

Lakini
alisema kuwa Netanyahu ataungwa mkono na Marekani “kumaliza kazi ya
kuharibu tishio la Hamas” ikiwa Hamas haitakubali mpango huo.

Netanyahu
kisha akasema Israel “itamaliza kazi” ikiwa Hamas itakataa mpango huo
au haitaufuata.

Soma zaidi:

Unaweza kusoma;

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *