
Chanzo cha picha, Getty Images
Tottenham ni miongoni mwa timu zinazowania saini ya beki wa Crystal Palace na Uingereza Marc Guehi, 25. (CaughtOffside)
Meneja wa Tottenham Thomas Frank anataka kumleta mlinzi wa Jamhuri ya Ireland Nathan Collins, 24, kutoka Brentford. (TBR Football)
Kiungo wa kati wa Tottenham na Uruguay Rodrigo Bentancur, 27, anakaribia kukubaliana kandarasi mpya na klabu hiyo ya London. (Football.London)

Chanzo cha picha, Getty Images
Habari za ndani ya Manchester United zinahofia meneja wa Ureno Ruben Amorim, 40, atajiuzulu kabla ya kutimuliwa. (iPaper)
Kiungo wa kati wa Real Madrid na Uruguay Dro Fernandez, Federico Verlvade, 27, analengwa na Manchester United mwaka ujao. (Fichajes – In Spanish)
Kiungo wa kati wa Barcelona na Uhispania Dro Fernandez, 17, hana nia ya kusikiliza ofa kutoka nje ya nchi, licha ya klabu za Arsenal, Chelsea na Manchester City kumataka. (TBR Football)

Chanzo cha picha, Getty Images
Fulham wanapanga kumnunua kiungo wa Middlesbrough Muingereza Hayden Hackney, 23. (Football league World)