#HABARI: Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), imeteketeza jumla ya kilogram 4,402.02 za Dawa za Kulevya katika kiwanda cha Saruji cha Twiga, kilichopo Wazo, jijini Dar es Salaam.
Dawa zilizoteketezwa ni pamoja na kilogramu 2,168.18 za methamphetamine, kilogramu 1,064.29 za Heroin, gramu 326.95 za cocaine, kilogramu 515.48 za bangi na kilogramu za mirungi.
Dawa hizi zilihifadhiwa kama vielelezo vya mashauri mbalimbali yaliyoko Mahakamani, ambapo baadhi ya mashauri bado yanaendelea kusikilizwa huku mengine yakiwa tayari yametolewa hukumu.
Kwa mashauri ambayo bado hayajakamilika, Mahakama iliagiza dawa hizo kuteketezwa kutokana na hatari ya kuharibika au kubadilika umbo, kwa mujibu wa Sheria ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya ya mwaka 2015, inayotaka vielelezo vya dawa za kulevya kuharibiwa wakati shauri linaendelea au baada ya hukumu kutolewa.
Miongoni mwa Mashauri yaliyohusiana na dawa zilizoteketezwa ni kesi ya Najimu Abdallah Mohamed, iliyohusisha heroin kilogramu 882.71 na methamphetamine kilogramu 2,167.29, ambayo bado yanaendelea.
Aidha yapo Mashauri yaliyokwishatolewa hukumu ikiwemo ya Hassan Azizi aliyepatikana na hatia ya Heroin gramu 983.5 na kuhukumiwa kifungo cha maisha, Salum Shaaban Mpangula aliyehukumiwa kifungo cha maisha, Hemed Juma Mrisho maarufu kwa jina la “Hororo” aliyehukumiwa kifungo cha maisha, pamoja na kesi ya Ramadhan Shaban Gumbo, aliyehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela, na Irene Dockson Mseluka aliyehukumiwa miaka mitano na Gema Victor Mmasy aliyehukumiwa miaka mitatu.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KISHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.