
Chanzo cha picha, Getty Images
Uongozi mkuu wa Real Madrid una shaka kuhusu kutafuta dili la kumnunua mlinzi wa Liverpool na Ufaransa Ibrahima Konate, 26, ambaye mkataba wake unamalizika Anfield msimu ujao. (Fichajes – In Spanish)
Liverpool wamempanga beki wa kati wa Crystal Palace na Ufaransa Maxence Lacroix, 25, kama mbadala wa mchezaji mwenzake wa klabu, mlinzi wa Uingereza Marc Guehi, 25. (Football Insider)
Manchester United wamemuongeza kiungo wa kati wa Brentford na Ukraine Yehor Yarmolyuk mwenye umri wa miaka 21 kwenye orodha ya wachezaji wanaolengwa na uhamisho. (Caughtoffside)
Mshambulizi asiyekubalika wa Manchester United Joshua Zirkzee bado ana nia ya kutaka kujiunga na Juventus na AC Milan, huku mchezaji huyo wa kimataifa wa Uholanzi, 24, pia akilengwa kwa mkopo Januari na klbau ya Como. (ESPN), nje

Chanzo cha picha, Getty Images
Manchester United wamekamilisha mpango wa kumsajili kiungo wa kati wa Colombia Cristian Orozco, 17, kutoka klabu ya Bogota Fortaleza. (Fabrizio Romano),
Tottenham na Manchester United wako mbele ya Fulham katika mbio za kumsajili kiungo wa kati wa Middlesbrough Muingereza Hayden Hackney, 23. (TeamTalks)
Newcastle wanamtaka kiungo mshambuliaji wa Athletic Club mwenye umri wa miaka 25 Oihan Sancet. (Mundo Deportivo – In Spanish)
Real Madrid watamfikiria kiungo wa kati wa Paris St-Germain na Ufaransa Warren Zaire-Emery, 19, kama mchezaji anayelengwa na kiungo wa kati wa Manchester City na Uhispania Rodri, 29. (Fichajes – In Spanish)

Chanzo cha picha, Reuters
Arsenal, Manchester City, Real Madrid na Barcelona ni miongoni mwa klabu maarufu zinazomfuatilia kiungo mshambuliaji wa Klabu ya Tijuana mwenye umri wa miaka 16 kutoka Mexico Gilberto Mora. (TeamTalks),
Beki wa Liverpool wa Italia Giovanni Leoni, 18, hatarajiwi kurejea uwanjani hadi mwisho wa 2026 kufuatia upasuaji wa kano za goti. (Mail – Subscription Required),
Uvumilivu wa mshambuliaji wa Manchester City Erling Haaland katika hali ngumu ya klabu hiyo unazidi kuzorota, licha ya mchezaji huyo wa kimataifa wa Norway, 25, kusaini mkataba mnono hadi 2034. (Star)
Aliyekuwa mkurugenzi wa muda wa michezo wa Liverpool Jorg Schmadtke anapangwa kuchukua nafasi sawa na Borussia Monchengladbach. (Kicker – In Deutch)

Chanzo cha picha, Getty Images
Kiungo wa kati wa Manchester City Phil Foden, 25, anashinikiza kuorodheshwa tena katika timu ya England, lakini winga wa Everton anayecheza kwa mkopo City Jack Grealish, 30, anaonekana kukosa nafasi. (Guardian).