
Shambulio hilo limetokea nje ya sinagogi katika siku ya Yom Kippur, inayotajwa kuwa siku takatifu zaidi katika kalenda ya Kiyahudi na limezua maswali kuhusu usalama wa jamii za wachache katika nyakati za ibada.
Kwa mujibu wa taarifa ya polisi wa Manchester, mshambuliaji aliuawa kwa kupigwa risasi na maafisa wa usalama wakati wa tukio hilo, huku washukiwa wengine watatu wakikamatwa.
Taarifa ya polisi imeongeza kwamba wamemtambua mshambuliaji huyo kuwa Jihad Al-Shamie, raia wa Uingereza mwenye asili ya Syria, mwenye umri wa miaka 35.
Polisi imetangaza tuko hilo kuwa la kigaidi na wanaendelea na uchunguzi kubaini nia ya shambulio hilo.
Vikosi vya usalama vimeimarisha ulinzi katika maeneo ya ibada kote Uingereza.