Jeshi la Polisi Mkoa wa Ruvuma linawashikilia watu 15 kwa tuhuma za kuhusika na mauaji ya watu watano yaliyotokea wilayani Tunduru.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, SACP Marco Chilya, miili ya marehemu ilikutwa katika maeneo tofauti ikiwa na majeraha ya kukatwa na kuchomwa na vitu vyenye ncha kali.
Amesema chanzo cha tukio hilo ni mzozo uliotokea kati ya mkulima na mfugaji katika kijiji cha Wenje, ambapo inadaiwa wawili hao walipishana kauli, hali iliyochochea ugomvi mkubwa uliosababisha vifo hivyo pamoja na majeruhi watatu.
Watuhumiwa 15 wa tukio hilo wamekamatwa na uchunguzi wa kina unaendelea ili kubaini wahusika wote na kuchukua hatua za kisheria.
#AzamTVUpdates
Mhariri | John Mbalamwezi