Manowari ya kifaransa yenye uwezo maalum wa kujihami dhidi ya mashambulizi ya anga imeanza mazoezi maalum yanayojulikana kama “Wildfire 2025” katika Bahari ya Mediterania.

Kwa muda wa siku tano, wanamaji wa kifaransa wanajifunza mbinu mbalimbali za kukabiliana na vitisho vya anga, ikiwemo kupiga risasi kuelekea ndege zisizo na rubani (drones) zinazokuja kwa kundi au moja moja, pamoja na kufanya majaribio ya vita vya kielektroniki dhidi ya ndege zinazofanana na makombora au ndege za kivita.

Mazoezi haya yanachukuliwa kuwa sehemu muhimu ya maandalizi ya jeshi la majini la Ufaransa katika kukabiliana na tishio la drones za kivita ambazo zinatumika zaidi kwenye migogoro ya kisasa. Kupitia “Wildfire 2025”, jeshi hilo linatarajia kuboresha uwezo wake wa kugundua, kudhibiti na kuharibu malengo madogo ya angani kabla hayajasababisha madhara.

#AzamTVUpdates
Mhariri | John Mbalamwezi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *