Wadau wa elimu nchini wamehimizwa kuwekeza katika kuongeza motisha ya kujifunza kwa watoto sambamba na kukuza hali ya ufundishaji kwa waalimu, ili kuongeza ubora wa elimu na kufanikisha malengo yaliyoainishwa katika sera ya elimu.

Rai hiyo imetolewa jijini Dar es Salaam na Zakayo Mlenduka, Afisa Elimu wa Awali na Msingi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo, wakati wa kutoa medali na zawadi kwa wanafunzi waliofanya vizuri katika mtihani wa kujipima ulioandaliwa na Taasisi ya Teachers Junction, ambao ulifanywa na wanafunzi wa darasa la nne, sita na saba.

#AzamTVUpdates
✍Estabela Malisa
Mhariri | John Mbalamwezi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *