Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru 2025, Ismail Ally Ussi, amezitaka halmashauri nchini kutenga na kupima maeneo kwa mpangilio bora ili kupunguza migogoro ya ardhi.
Amesisitiza wananchi wenye viwanja kuhakikisha wanakuwa na nyaraka halali za umiliki, akisema hatua hiyo itasaidia kuepuka migogoro inayojitokeza baada ya wamiliki kufariki dunia.
Kauli hiyo ameitoa baada ya kuzindua mradi wa upimaji wa viwanja katika kijiji cha Mbebe, wilayani Ileje, mkoani Songwe, ambapo Mwenge wa Uhuru unaendelea na mbio zake.
✍ Joyce Lyanda
Mhariri @claud_jm
#AzamTVUpdates